Kiswahili KCSE Practice Exam (2006)


July 2, 2011 Facebook Twitter LinkedIn Google+ KCSE Exams


INSHA
Saa 1 3/4
Andika insha mbili.Swali la kwanza ni la lazima.
Kisha chagua insha moja nyingine kutoka hizo tatu zilizobaki.
Kila insha isipungue maneno 400.
Kila insha ina alama 20.
1. Umeteuliwa kuwa katibu wa kamati inayotoa mapendekezo ya jinsi ya kupambana na tatizo sugu la dawa za kulevya.Andika ripoti yako.
2. Ukubwa ni jaa.
3. Malizia kwa….Wekundu wa uchwejua ulienea kila mahali;anga nzima ilijaa wekundu kama kwamba mazingira yalipatana na hali iliyokuwako.Kwa mbali niliisikia sauti iliyonikumbusha maneno niliyoambiwa zamani.Laiti ningeyasikiliza maneno hayo.
4.”Utandawazi una athari mbaya katika maisha yetu.”Jadili.

Karatasi 3
FASIHI
Saa 2 ½
Jibu maswali manne pekee.
Swali la kwanza ni la lazima.
Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani:
Tamthlia,Riwaya,Hadithi Fupi na Ushairi.Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
FASIHI SIMULIZI
1.(a) Fasihi Simulizi ni nini?(alama 2)
(b) Eleza tofauti nne baina ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi.(alama 12)
(c) Nini umuhimu wa Fasihi Simulizi?(alama 6)

TAMTHILIA
Kithaka wa Mberia:Kifo Kisimani
2. “Utani? Haukuwa utani! Mtemi amesikia sifa za uzalendo wako…..Mipango yote imepangwa na kupangika….Unajua,bwana,hiari ya binadamu ni kifaa cha mtu mwenyewe.Anaweza kukitumia vizuri au vibaya.Anaweza kukitumia kujinufaisha maishani au kujikwamisha njiani.Inategemea mtu mwenyewe”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 2)
(b) Ni mipango gani inayozungumziwa?(alama 4)
(c) Fafanua jinsi baadhi ya wanajamii wa Kifo Kisimani wanavyoitumia hiari yao vibaya.(alama 14)

RIWAYA
Z.Burhani:Mwisho wa Kosa
3.Linganisha wasifu wa wahusika wafuatao na uonyeshe umuhimu wao katika riwaya ya Mwisho wa Kosa:
(a) Monika
(b) Muna (alama 20)

HADITHI FUPI
K.W.Wamitila:Mayai Waziri wa Maradhi
Jibu swali la 4 au la 5.
Siku ya Mganga
4. “Lakini kulikuwa na tatizo gani iwapo….mganga alikuwa hajui chochote kuhusu ugonjwa?”
(a) Fafanua muktadha wa maneno haya.(alama 2)
(b) Eleza sifa za mganga anayerejelewa katika hadithi hii.(alama 10)
(c) Taja na ufafanue madhara aliyosababisha mganga kwa jamii.(alama 8)

7.Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata.
MKULIMA
Mtazameni….nguzo ya Afrika
Mtumwa wa watumwa waloridhiya!
Amekita jembe lake akilisujudia
Kwa tambo liloumbuka na kuselehea
Uso ukifuka ukata ulojifanya tabia
Na machungu ya maonevu alovumilia.

Moyo wake mzito ulokokomaa kama kuni
Haujui tena kutarajia wala kutamani
Umekufa ganzi,kutohisi raha wala huzuni

Basi iteni fikira mambo mukiyafikiri
Siku hamaki yake itapochafuka kama bahari
Siku ukweli wa hali yake utapodhihiri
Umejiandalia vipi…..
Huo mkono ulomuumba na kumkausha
Hizo pumzi zilomzimia taa ya maisha
Kumfunga kizuizi,gizani kumtowesha?

Ni jawabu gani alowekewa na wakati
Kipoza ghadhabu ya kiu ingawa katiti
Kuiliwaza hamaki ya njaa hii ya dhati
Njaa ya maisha itakayo kushibishwa.
(a) Eleza mambo muhimu yanayojitokeza katika shairi hili.(alama 4)
(b) Taja na utoe mifano ya aina zozote mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili.(alama 4)
(c) Eleza umbo la shairi hili.(alama 3)
(d) Onyesha umuhimu wa matumizi ya kihisishi katika shairi.(alama 2)
(e) Fafanua maana ya:
(i)Siku hamaki yake itapochafuka kama bahari.(alama 2)
(ii) kuipoza ghadhabu ya kiu ingawa katiti.(alama 2)
(f) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi:
(i)tambo
(ii) ulokokomaa
(iii) kumtowesha (alama 3)

For our Complete List of KCSE SAMPLE EXAMS – Click HereRating: 0.8/5. From 2 votes.
Please wait...
Comments