KCSE-2008-Kiswahili-Paper-3


July 16, 2011 Facebook Twitter LinkedIn Google+ KCSE Exams


1       (LAZIMA)                       USHAIRI

Soma shairi hili ujibu maswali yanayofuata.

                        WASAKATONGE

1.                    Wasakatonge na juakali

Wabeba zege ya maroshani,

Ni msukuma mikokoteni,

Pia makuli bandarini,

Ni wachimbaji wa migodini,

Lakini maisha yao chini.

2          Juakali na wasakatonge

Wao ni manamba mashambani,

Ni wachapa kazi viwandani,

Mayaya na madobi wa nyumbani,

Ni matopasi wa majanni,

Lakini bado ni masikini.

3          Wasakatonge na juakali

Wao huweka  serikalini,

Wanasiasa madarakani,

Dola ikawa mikononi,

Wachaguliwa na ikuluni,

Lakini wachaguaji duni.

4          Juakali na wasakatonge

Wao ni wengi ulimwenguni,

Tabaka lisilo ahueni,

Siku zote wako matesoni,

Ziada ya pato hawaoni

Lakini watakomboka lini?

(Mohammad Seif Khatib)

(a)  “Shairi hili ni la kukatisha tama”. Fafanua rai hii kwa kutoa

mifano mine.                                           (alama 4)

(b)   Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima na

uonyeshe mifano miwili ya jinsi ilivyotumika.   (alama 3)

(c)    Eleza umbo la shairi hili.                                    (alama)

(d)   Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari.   (alama 4)

(e)    Onyesha mifano miwili ya maadili yanayyojitokeza

Katika shairi hili.                                             (alama 2)

(f)     Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumi wa

katika shairi.

(i)         Manamba

(ii)        Tabaka lisilo ahueni                            (alama 2)

 

                              TAMTHILIA

Jibu swali la 2 au la 3.

Kithaka wa Mberia:  Kifo Kisimani

2          Ukitumia mifano, onyesha matumizi matano ya mbinu ya

ishara kama ilivyotumiwa katika tamthilia ya Kifo Kisimani.

(alama 20)

3          “Kwa hakika, Kama mzazi hana Kifani Katika Butangi nzima.

nap engine hata Katika ulimwengu mzima”.

(a)     Eleza muktadha wa dondoo hili.                                  (alama 4)

(b)     “Watu waliojiita washauri wa mtemi Bokono walikuwa si

washauri halisi bali wanafiki waliomdanganya.” Thibitisha Kauli

hii Kwa Kutoa mifano mitano.                  (alama 16)

 

                               RIWAYA

Jibu swali la 4 la 5.

Z. Burhani: Mwishi wa kasa.

4          “Wanawake Katika riwaya ya mwisho wa kasa wamepewa

nafasi ndogo katika masuala ya maendeleo ya Kijamii”

Thibitisha kauli hii Kwa Kutoa mifano kumi.          (alama 20)

5          Eleza jinsi wahusika wafuatao wanavyoafiki anwani ya

riwaya ya mwisho wa kosa:

(a)        Ali                                                        (alama 10)

(b)        Asha                                                    (alama 10)

 

                                             HADITHI FUPI

            K.W. Wamitila (mhariri):     Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine

6          “Umdhaniaye ndiye, Kumbe siye”.

Kwa Kurejelea hadithi sosote tano Katika diwani ya mayai waziri wa

maradhi na hadithi nyingine, onyesha ukweli wa kauli hii.       (alama 20)

 

                                             FASIHI SIMULIZI

7          FAFAnua Sifa ZOZOTE kumi za mtambaji bora wa ngano.             (alama 20)No votes yet.
Please wait...
Comments