KCSE-2008-Kiswahili-Paper-2


October 17, 2015 Facebook Twitter LinkedIn Google+ KCSE Exams


1       UFAHAMU

Soma makala yafuatayo kasha maswali.

Kuna aina kuu za hisia zinazotawala na kuongoza maisha ya mwanadamu:Kuona, Kusikia,

Kugusa, Kuonja na kumusa.Ni vigimu kusema ni hisia gani muhimu kuzidi nyingine ingawa ni dhahiri

athari kubwa humuangukia mahuluku asiyeweza kuona.inasemekana kuwa mishipa ya fahamu

inayounga ubongo na macho ni mikubwa zaidi kuliko mishipa ya fahamu inayounga ubonga na

viwambo vya masikio.Nakatika maisha na nyendo za kila siku kuona hupewa uzito mkubwa

minghairi ya kusikia .pengine basi sio ajabu, kama itakavyobainika punde baadaye,kuwa kazi

nyingi za fasihi andishi zimeelemea mno katika hisia  hii kana kwamba zile nyingine kuu hazipo kabisa

Hakika hili ni kosa .Maana kusika kugusa, kuonja, na kunusa nako ndiko  humkamilsha mwanadamu

aweze kuyafaidi maisha yake.Nahata mbele ya sheria, ushahidi huweza kutolewa mintaarafu ya

kusikia, kugusa, kuonja na kunusa alimardi shahidi awe amesikia, kugusa ,kuonja au kunusa

mwenyewe.ushahidi wa kuambiwa haukubaliwi.

Kwa hivyo basi kazi ya sanna ambayo itazituma fikira za msomajji zihisi kuona, kusikia, kuonja,

kugusa, na kunusa matendo na mazingira yanayousimuliwa humpeleka msomaji huyo katika mipaka na

Nyanja za juu za ufahamu na furaha.

kila hisia ina umuhimu wake kutokana na mmazingrira ya tukio linalohuska au kusimuliwa.

Maana kazi zote za sanaa hutokana na matendo na maisha ya watu ambao katika matuko, visa na mazingira yao hutumia hisia zao zote tano ama kwa pamoja au kwa nyakati mbalimbali. Ili basi msomaji aweze kupata mandhari kamili, na hata yeye mwenyewe ashiriki katika matukio yenyewe kwa kuchukia, kuonea huruma, n.k., muhimu, kabla ya yote, apate hisia zote hizo tano. Kazi ya sanaa inayojihusisha na hisia moja tu au mbili huwa muflisi kisanii kwa vile inashindwa kuwailisha kwa sababu ya sauti ndogo tu ya ndege aliaye pekee nyikani, au nyimbo ya zamani? Sauti ya ndegehuwea kuleta majonzi ya miaka mingi mno ya utotoni wakati ambapo mtu alifiwa na mzazi, ndugu, jamaa au sahibu wake. kadhalika nyimbo ya kale huweza kuchimbua ashiki ya zamani baina ya wapenzsi, au kutonesha jeraha la masaibu na madhila yaliyopita. Na wala sio nyimbo na sauti ya ndege tu, pengine hata harufu ya maua huwa na nguvu za kumbakumbu kubwa mno.

Licha ya yote hayo, matumizi ya hisia nyingi yanasaidia kujenga mandhari kamili ya tukio

katika akili ys msomaji. mathalan badala ya kuelezwa tu kuwa paliandaliwa chakula kizuri,msomaji

anaelezwa vitu ambavyo vimeandaliwa na kuelewa vyema zaidi kwa kuambiwa mtu Fulani

alikuwa na wajihi wa kutisha, huelezwa na kuelezwa  vyema zaidi kwa kuainishia jinsi pua,macho, rangi,

nyweli , mdomo na meno ya mtu huyo yalivyo. Na hivyohivyo kwa mifano mingine kadha wa kadha kama vile hasira na ucheshi. Kutokana na maelezo ya kutosha ya hisia msomaji huweza kumuashiki janabim,  au akadondokwa na ute kutamani chakula ambacho hakipo mbele yake.

Na sio hivyo tu. Hisia zinazotumiwa kutokana na hisia mbalimbali na wala sio kauli za mkatomkato za mwandishi kama ilivyogusiwa hap juu. Kauli za mkatomkato sio tu hadumaza sanaa, bali pia hudhalilisha hata akili ya msomaji: kwani umbuji wa mwandishi ni pamoja na kufanya matendo na mazingira anayoyasimulia yawasilishe na kuwakilisha fikira za wahisika wake na hata zake mwenyewe.

Hivyo ni dhahiri kuwa hisia humsaidia msomaji kuzama katika matendo na kuelewa fikra za mwandishi mwenyewe, asili na makazi yake, kuwadadisi na kuwaelewa wahusika wenyewe, n.k.

 

Makalla kutoka:                                                Saffari, A.J. ‘Hisia Katika Fasihi Andishi’

                                                                                                                Katika Mulokozi, M.M na Mung’ ong’o (Wah.)

                                                                                                                (1993:33) Faisihi, uandishi na uchapishaji

Dar-es-Salaam: Dar-es-Salam Univ. Press

 

(a)  taja na ueleze uwanja ambao hutilia mkazo hisia zote. (alama 3)

(b)  kwa mujibu wa kifungu hiki, ni nini matokeo ya kusisitiza hisia ya kuona katika fasihi

andishi ? (alama 2)

(c)  (i)  mwandishi ana maoni gani kuhusu kazi nzuri ya sanaa. (alama 2)

(ii)  Maoni hayo yana umuhimu gani? (alama 4)

 

(d)  Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika kifungu ulichosoma.

(i)           muflisi kisanii………………………………………………………………………………………

(ii)          Jeraha la masaibu……………………………………………………………………………….

(iii)         Kumuashiki janabi………………………………………………………………………………

 

(iv)         umbuji………………………………………………………………………………………………..

(alama 4)

2 UFUPISHO

Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za

kiuchumi ghairi ya zile ambazo ni za lazima kwa serikali au dola kama ulinzi, sheria na mpangilio

mzima wa jamii, huwa huria kwa watu binafsi.misingi wa soko huria, sifa kuu ya utandawazi, ni kuibua

na kudumisha mazingira na hali zinazochochea na kumruhu mtu yeyoto kuongozwa na hawaa, au

matamanio ya kibishara anayoyaona sawa pasi na hofu ya kuingilwa na udhibiti wa swrikali.

mazingira hayo yanawapa watu satua ya kufanya maamuzi kuhusu hatima yao ya kiuchumi,

uamuzi kuhusu suala la ajira yao, matumizi ya mataji-kipato na harija zake, na uwekezaji mzima.suala

mojawapo linaloibuka kuhusiana na mfumo wa soko huria ni kuweka mipaka bainifu na wazi baina ya

amali na shghuli zinazohusishwa na serikali na zile ambazo huachwa huria kwa watu.kwa mfano

inaaminiwa kuwa haki ya kuishi na kulindwa sdhidi ya shambulizi, liwe la kijambazi au la kigaidi, ni ya

kimsingi za afya nazo zinaingia katika kumbo hili.ikiwa huduma hizi zitaachwa huria pana uwezekano

mkubwa kuwa zitaishia kuwa istihaki ya wenye mtaji na kipato cha juu tu.

licha ya kuwepo kwa sheria au kanuni huria kutoka  Nyanja maalum.hutokea hali ambapo

udhibito wa kiserikali ni lazima.hili hutokea pale ambapo ipo haja ya kuyalinda mazingira hasa

kutokana na uchafuzi wa viwanda au tasnia.aidha udhibiti huo ni lazima pale ambapo haki za watu

wengine zinahusika:yaani ikiwa uhuru wa hata mtu mmoja unaadhirika kuotokana na sera hizo.pana

haja ya kuingilia ili kuisawazisha hali yenyewe.

(a)  Andika kwa muhtasari maana ya uchumi wa soko huria kulingana na taarifa hii.

(maneno 25-30)      (alama5. 1 ya mtiririko)

Matayarisho

Jibu

(b)  Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika aya ya pili nay a tatu.

(maneno 70-75)      (alama 10.3 za mtiririko)

Matayarisho

Jibu

 

3       MATUMIZI YA LUGHA

(a)  Tambua mzizi katika neon

“msahaulifu” ………………………………………………………………………………………..(alama 1)

(b)  Tunga sentensi ukitumia kivumishi cha momino.  (alama 1)

(c)  Andika kinyume  cha:

Wasichana watatu wanaingia darasani kwa haraka.  (alama 2)

(d)  (i)  Fafanua maana ya “mofimu huru”.  (alama 1)

(ii)  Toa mfano mmoja wa mofimu huru.  ((alama 1)

(e)  Tambua kiambishi awali na tamati katika neon alaye.  (alama 2)

(f)  Tumia kirejeshi-amba kuunganisha sentensi zifuatazo:

(i)  Mwanafunzi Yule ni mrefu.

(ii)  Mwanafunzi Yule amepita mtihani.  (alama 2)

(g)  sahihisha sentensi hii:

Waya yangu imepotea……………………………………………………………(alama 1)

(h)  Taja aina ya yambwa iliyopigiwa mstari katika sensensi ifuatayo:

Mpishi amempikia mgeni wali vizuri.  (alama 1

(i)  Neno “chuo” lina maana ya “shule inayotoa mafunzo maalum ya kazi fulani”.

Tunga sentensi mbili kubainisha matumizi mengine mawili ya neon hili. (alama 2)

(j)  Ibadilishe chagizo ya mahali kwa ile ya wakati katika sentensi ifuatayo:

Mchezaji aliucheza mpira mjini makindi.  (alama 1)

(k)  Eleza maana mbili za sentensi:

Yohana alimpigia husha mpira.  (alama 2)

(l)  kanusha:

sisi tumemaliza kujenga nyumba ambayo ingalikuwa yake angalifurahi. (alama 1)

(m)  unda nomino kutokana na:

(i)  Zingua …………………………………………………………………………………………(alama 1)

(i)  Tosa …………………………………………………………………………………………….(alama 1)

(n)  Ichoree vielezo matawi sentensi:

Paka mdogo amepanda mchungwani.  (alama 4)

(o)  Tumia kihusishi badalia kutunga upya sentensi hii:

Mgeni yuko katika nyumba.  (alama 1)

(p)  unda kitenzi kutokana na neon “sahili” ……………………………………………………..(alama 1)

(q)  Eleza tofauti kati ya sauti (Z) na [d]  (alama 2)

(r)  Tambua aina ya kitenzi kilichopigiwa mstari katika sentensi.

Mzee huenda anacheza kamari.  (alama 1)

(s)  badilisha kiwakilishi kimilikishi kwa kiwakilishi kionyeshi katika sentensi:

Chake kilipatikana nchini.  (alama 1)

(t)  Tumia mfano mmoja kutofautisha baina ya sentensi sahili na ambatano. (alama 4)

(u)  Tunga sentensi itakayodhihirisha matumizi ya kielezi cha nomino.  (alama 1)

(v)  andika kwa wingi :

Mvua imebomoa nyumba ya jirani.  (alama 1)

(w)  Akifisha kifungu kifuatacho:

huends serikali iwazie kuidhibiti bei ya petrol hatuwezi kuyaruhusu makampuni ya

petrol kuunyanyasa umma alisema waziri wa kawi bei ya petrol imeongezwa mara nne

katika kipindi cha mwezi mmoja.  (alama 4)

 

4 ISIMU JAMII

Eleza huku ukitoa mifano sifa tano za kimsingi zinazitambulisha sajili ya mazungumzo. (alama 10)

 

 Rating: 4.0/5. From 2 votes.
You voted 5, 2 months ago.
Please wait...
Comments